"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Ni moja ya mafungu maarufu na pendwa
sana miongoni mwa watu, lakini hata hivyo bado hatuelewi vizuri mstari unaosema akamtoa
mwanawe pekee , Kimsingi shetani alijua wazi kuwa hakuna njia ambayo Mungu angefanya
kumuokoa mwanadamu aliyeanguka dhambini ila tu kwa kupitia uzao wa mwanadamu kitu
ambacho alijipa matumaini kuwa tendo hilo haliwezekani kwasababu mosi, Mwanadamu mwenye
dhambi hawezi kumuokoa mwenye dhambi mwenzake inahitajika mwanadamu mtakatifu asiye na
dhambi kufanya hivyo. Pili, na kutokana na sababu hio hata Mungu katika wake hawezi kumuokoa
mwanadamu katika hali ya uungu maana sharti ni kwamba damu lazima iokoe damu na Mungu
sio binadamu maana pia hakuna binadamu atakayeweza kumuona Mungu akaishi, kwasababu hio
basi Yesu akafanyika kuwa mwana wa Mungu, akauvaa ubinadamu ili aweze kupata kibali cha
kuweza kumkomboa binadamu maana tayari amekidhi vigezo vyote yaani yu katika hali ya
kibinadamu pili hana dhambi (Wafilipi 2:6-8).
Huu ndio utoaji bora zaidi kuwahi kutokea katika dunia. Leo hii hatuwezi kujitoa uhai lakini
tunaweza kutoa fadha, muda, mali, akili nk kupitia Zaka na Sadaka katika namna
ambayo inakubalika na mbingu. Karibu tujifunze namna ya kumtolea Mungu Zaka na Sadaka.

