Sura za 38 & 39 za kitabu cha Ezekieli kimeleta mgongano mkubwa wa kufasiriwa kwa ufasaha ni nini maana ya vita ya Gogu na Magogu kwasababu imekuwa ikihushishwa na kutokea kwa vita ya tatu vya dunia baina ya mataifa makubwa matatu Marekani , Urusi na China (pamoja na mataifa yanayolenga mlengo wa kulia au kushoto wa siasa za kibepari dhidi ya zile za kikomunisti).
Ufasiri wa Moja kwa moja wa juu ya nchi zinazotajwa kuwa chini ya Gogu yaani, Roshi (Russia - Urusi), Mesheki (Moscow) na Tubali (Turkey- Uturuki) unachukuliwa moja kama kigezo cha kuchochea vita vya tatu vya dunia. [Marshalling Of The Nations: Alonzo T Jones, 1900]
Hata hivyo Gogu na Magogu hazitajwi tu katika Ezekieli bali hata katika Mwanzo na Mambo ya Nyakati, zikitwaja kama majina ya watu yaani Magogu alikuwa mjukuu wa Nuhu na Gogu anatajwa kuwa mwana wa Yoeli. Hii inafanya kuweka ugumu wa kujua je Gogu na Magogu ni nchi, majina au sehemu, vita hii itapiganwa lini na nini itakuwa sababu ya vita hivyo?

