Maisha yana misimu! kama jinsi ambavyo dunia ina misimu minne inayoitwa majira ya mwaka, vivyo hivyo binadamu pia tunapitia misimu ya vipindi mbalimbali katika maisha, jana haiwezi kuwa sawa na leo na kesho pia haiwezi kuwa sawa na leo.
Vipo vipindi vitatu ambavyo kila mwanadamu huvipitia katika wakati wake chini ya jua, vipindi hivi si vigeni vinachukua sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku,
Si ajabu kuanzia mwanzo 1-2 (Sura mbili tu) maisha yanaonekana ni mazuri, kuanzia mwanzo 3- ufunuo 20 (Sura nyingi sana) maisha ni magumu kweli kweli yasiyoeleweka halafu ufunuo 21-22 (sura mbili tu) maisha yanarudishwa tena kuwa mazuri.
Kwa kuangalia huko tunaona vipindi vitatu ambavyo hata kitabu cha Zaburi (Ketuvim "The Writtings") kinazionyesha, ndio maana Zaburi 1 inaanza kwa utii kana kwamba mwandishi yupo kwenye maisha mazuri na Zaburi 150 inamalizia kwa furaha nyingi sana kana kwamba mwandishi ametoka kwenye shida nyingi.
Vipindi hivi vitatu ni ;
1. Orientation (Wakati wa furaha) - wakati ambao biashara zinaenda, umepata mke/mume, umefaulu mtihani wa mwisho, umepata kazi, afya iko bingo yan mambo ni barabara.
2. Dis Orientation (Wakati wa shida) - huu ndio wakati ambao Mungu anaonekana hajali, hajibu maombi, magonjwa yamekuandama, umeachwa na mwenzi wako, mtihani umefeli, ule mchongo uliokuwa unautegemea umefeli yani mambo ni mvurugano kweli kweli.
3. Reorientation/ New Orientation (Wakati baada ya shida) - wakati huu Mungu amekutoa kwenye shida zako na unafuraha na imani kupitia yeye.
Mara nyingi hatupendi kukubaliana na kipindi cha mpito kutoka kweny ORIENTATION kwenda kwenye DISORIENTATION kwasababu tunaigiza maisha na hatupendi kukubaliana na ukweli kuwa maisha hayawezi kuwa sawa siku zote na lazima tukubali kuugua na huzuni. John Fitzgerald Kennedy aliwahi kusema "Victory has thousand of fathers but defeat is an orphan"
Lakini pia hatupendi kukubaliana na kipindi cha kutoka kwenye DISORIENTATION kwenda kweny NEW ORIENTATION kwasababu hatua hii inahitaji kukubaliana na uhalisia,kuanza maisha mapya,kuachana na mtindo wa maisha wa zamani na kutegemea tumaini.

