Wakati mmoja Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Alphabet (kampuni mama ya Google , YouTube nk) Sundar Pichai aliwahi kunukuliwa akitoa risala fupi ya sekunde sitini akisema;
"Kama maisha yangechukuliwa mfano wa mtu anayerusha matufe matano hewani,manne yaliyoundwa kwa udongo na moja lililotengenezwa kwa mpira ,kiasi cha kwamba anatakiwa ajitahidi matufe hayo yasianguke yakagusa ardhini,na ikiwa matufe hayo yakaandikwa na kupewa majina "Kazi,Afya,Familia,Nafsi,Uhusiano na ndugu", basi isingemchukua mtu muda kutambua kuwa tufe lililotengenezwa kwa mpira ni kazi ,kwasababu kwa ikiwa kwa bahati mbaya likitua ardhini litadunda na kurudi tena hewani kwakuwa ni rahisi kubadilisha kazi lakini yale matufe mengine yakitua ardhini kwa namna yoyote yataharibika ama kuvunjika na hayawezi kuundwa kurudi kama zamani ,ndivyo ilivyo juu ya afya ,familia ,nafsi na uhusiano na ndugu. Hivyo basi lazima tuwe makini na yale tunayoyatafuta ama kuhangaikia"
Afya ni kiungo muhimu katika maisha, hakuna jambo lolote linaloweza kukamilishwa na mtu hapa duniani kama afya yake ni mbovu. Lakini njia sahihi ipo, nayo ni ipi ?

