Wakati ubongo ukiwa kama mji mkuu kwa kuratibu mambo yote ya mwili, tumbo kama mji wa kibiashara kwa kufanya manunuzi ya kumeng'enya chakula, damu ikiwa kama wizara ya uchukuzi, Ulimi unasimama kuwa msemaji mkuu wa serikali ya mwili. Ni kiungo kidogo chenye nguvu ya kutafsiri ulivyo, unavyofikiri, unavyowaza na namna maisha yako yalivyo. Uwezo wa kutumia ulimi katika mazungumzo na kuongea ni moja ya ujuzi ambao watu wanaudharau. Wakati mmoja aliyekuwa mtendaji mkuu na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya PepsiCo Indra Nooyi aliwahi kunukuliwa akisema; "huwezi kuwekeza fedha kwenye mazungumzo" hapa alimaanisha kuwa mazungumzo ni ujuzi ambao unaweza kufanya kazi mahali ambapo fedha isingeweza kutumika. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher aliwahi kumuajiri mtu wa lugha ya katika ofisi yake ili aweze kumsaidia kuongeza ujuzi wake katika mazungumzo.
Unakumbuka jinsi Waziri Mkuu wa uingereza Winston Churchill alivyowashawishi waingereza kuelekea vita vya pili vya dunia kwa hotuba? Unaukumbuka uwezo wa Mwalimu Julius K Nyerere kutoa hotuba matata zenye kuteka hisia za wasikilizaji? Unakumbuka hotuba za redioni za Franklin Delano Roosevelt katika kuikoa Marekani dhidi ya anguko la kiuchumi zilizofanya kazi na kumfanya awe raisi pekee aliyeshika mihula minne ya uraisi wa Marekani? Unaukumbuka uwezo wa Steve Jobs kuelezea bidhaa za apple kwenye majukwaa "Product Presentations "? Unaikumbuka ile presentation yake ya Computer Apple Macintosh ilivyopelekea mauzo makubwa ?, Unawakumbuka Martin Luther King, Malcom X? Unakumbuka uweza wa Yesu Kristo katika mafundisho yake kukusanya watu wengi wamsikilize?
Yote hayo na mengineyo ya mfano wa hayo yameelezewa katika kitabu cha HEKIMA ZA MFALME SULEMANI.

